Tiwa Savage Akanusha Kuwahi Kutoka Kimapenzi Na Don Jazzy.

Mwanamuziki wa Nigeria, #TiwaSavage, amevunja ukimya kuhusu madai ya muda mrefu kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na #DonJazzy, bosi wake wa zamani wa lebo ya Mavins.

Kwa mujibu wa RoyalBlog, Tiwa alieleza kuwa madai hayo hayana msingi wowote na alisisitiza kuwa uhusiano wao ulikuwa wa kikazi tu. “Don Jazzy ni mtu mstaarabu sana ambaye alihakikisha kila kitu kinafanyika kwa weledi,” alisema Tiwa.

Akiendelea kueleza, Tiwa alikiri kwamba mara nyingi walifanya kazi usiku kucha wakiwa studio, na wakati mwingine alionekana akiwa amevaa mavazi yanayoweza kueleweka vibaya. Hata hivyo, Don Jazzy alichukulia hilo kwa utani na heshima, akimwambia, “Tiwa, tumeona haya yote, sio kitu kipya.”

Kwa kauli yake, Tiwa amefuta dhana potofu na kuwahakikishia mashabiki kuwa ushirikiano wake na Don Jazzy ulikuwa wa kazi tu bila mchanganyiko wa masuala ya kimapenzi.