TLS yataka Tundu Lissu aachiwe huru bila Masharti yoyote

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimetoa wito kwa serikali kumwachia huru mara moja na bila masharti yoyote Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Wakili Tundu A. Lissu, aliyekamatwa hivi karibuni.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumamosi, Aprili 12, 2025, Rais wa TLS, Wakili Boniface Mwabukusi, amesema kuwa kukamatwa kwa Wakili Lissu kunadhoofisha heshima ya taaluma ya sheria na misingi ya haki.

“Kuendelea kushikiliwa kwake kunaashiria vitisho kwa Wanasheria na washiriki wa siasa nchini,” ilisema taarifa ya TLS.

Chama hicho cha wanasheria kimeongeza kuwa iwapo wito wao hautazingatiwa, TLS inahifadhi haki ya kupendekeza kusitishwa kwa huduma za uwakilishi wa kesi za msaada wa kisheria (dock brief) na huduma nyingine za kisheria za kujitolea zinazotolewa na TLS na wanachama wake. Hatua hiyo inalenga kuwa njia ya amani ya kupinga vitendo vya unyanyasaji na mashtaka yenye mlengo wa kisiasa.

TLS pia imemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuhakikisha kuwa mashtaka mazito kama ya uasi yanayoandaliwa dhidi ya Wakili Lissu yanaungwa mkono na ushahidi madhubuti na hoja za kisheria. Chama hicho kimeonya kuwa uongozi wa kisiasa pekee hauwezi kuchukuliwa kuwa ni kitendo cha uasi kwa mujibu wa sheria zilizopo.

“Kukamatwa kwa Wanasiasa kinyume na sheria kunaweza kusababisha upinzani na machafuko,” ilionya TLS, ikizitaka mamlaka kuchukua hatua za kisheria na za tahadhari ili kudumisha amani na umoja wa kitaifa, na kuepusha hali ya hofu miongoni mwa wanasiasa kuelekea uchaguzi mkuu.

TLS imesisitiza wito wake wa kuachiwa huru mara moja na bila masharti yoyote Wakili Tundu A. Lissu, ikionya kuwa kuendelea kumshikilia kunadhoofisha misingi ya haki na kuashiria vitisho kwa wanasheria na wanasiasa nchin