Tory Lanez Adai Atatoka Jela Mwaka Huu 2025.

Tory Lanez Anasema Kwamba Ataachiwa Huru Kutoka Jela Mwaka Huu. Lanez Amesema Hayo Kwenye “Outro” Ya Album Yake Mpya “Peterson” Iliyotoka Tarehe 7 (Ijumaa) Wiki Iliyopita.

Album Hii Mpya Ya Tory Imegusia Zaidi Maisha Yake Binafsi Ikiwemo Kesi Yake Na Megan Thee Stallion, Maisha Yake Akiwa Jela, Amemchana Wakili Wake Wa Zamani Aliyemlazimisha Kutoa Ushirikiano Kwa Mamlaka kwenye kesi yake ili Kupunguziwa Adhabu N.k. Kwasasa Anatumikia Kifungo Chake Cha Miaka 10 Kwa Kosa La Kumshambulia Megan Kwa Risasi Julai 2020.