Trey Songz anachunguzwa kwa madai ya kumshambulia mpiga picha kwenye mgahawa huko New York.
Kwa mujibu wa TMZ, mhanga aitwaye Isaa Mansoor Anadai Kwamba Alipewa Kazi Ya Kuchukua Matukio Ya Trey Songz (Picha & Videos) kwenye mgahawa wa The Ivy siku ya Jumapili asubuh Huko New York, na anadai kuwa Trey Alifahamu Kabisa Uwepo Wa Camera Katika Eneo Hilo.
Imeripotiwa Kuwa Haikuwa Siku Nzuri baada ya Trey kukasirishwa na mashabiki waliokuwa wakimuomba kupiga naye picha. Wakati mmiliki wa mgahawa alipomwomba Trey apige picha ya mwisho mbele ya Logo ya mgahawa huo, Isaa anasema Trey ghafla alimchapa ngumi kichwani, akamsukuma ukutani, na kuvunja kamera zake mbili.
Mmiliki wa mgahawa alijaribu kuingilia kati, akimwambia Trey kwamba Isaa ni mtu wake, lakini Trey alijibu kwa hasira Na Kutojali Maneno Ya Mmiliki Wa Mgahawa Huo Na Kisha Kumkaribia Hadi mmiliki Mwenyewe kwa Kwa Hasira huku akimkunjia ngumi.
Isaa ambaye alikuwa ametoka hospitalini siku hiyo kabla ya tukio, anasema alipata Tatizo Kwenye ubongo, maumivu makali ya kichwa (migraine), na maumivu ya kifundo cha mguu (Ankle), Na Amesharipoti tukio hilo polisi, na mamlaka zimethibitisha kuwa uchunguzi umeanza.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.