Tristan, Justus & Diedo Star Watoa Ngoma Mpya Iitwayo ‘Inawauma’ – Wawa Tishio Uganda, Watarajiwa Kuwa Mastaa Wakubwa

Wasanii watatu chipukizi wenye njaa ya mafanikio—Tristan, Justus, na Diedo Star—wameungana na kutoa kazi mpya inayokwenda kwa jina la ‘Inawauma’, ngoma inayokuja kwa kasi na tayari imeanza kufanya maajabu, hususan nchini Uganda ambako imepokelewa kwa kishindo.

‘Inawauma’ ni ngoma yenye ujumbe mzito, ikiwasilisha hali ya kujivunia mafanikio licha ya maneno ya watu na changamoto za mitandaoni au maisha kwa ujumla. Wakiwa na mitindo ya kipekee na miondoko ya kuvutia, wasanii hawa wameonyesha wazi kuwa wana njaa ya mafanikio na wako tayari kuyashika majukwaa makubwa.

Kupitia uzinduzi huu, Tristan, Justus, na Diedo Star wamejijengea jina la kutajwa kama “the next big thing”—wakiwa tayari wamevuka mipaka na kuanza kuwika kimataifa. Katika muda mfupi tangu kuachia wimbo huo, wameanza ku-trend kwenye mitandao ya kijamii nchini Uganda huku wakionekana kuibua mjadala mzito miongoni mwa mashabiki wa muziki wa Hip-Hop na Bongo Fleva.

Wadau wa muziki na mashabiki wamekuwa wakifananisha uwezo wao na mastaa waliotangulia, na baadhi ya wachambuzi wa muziki wanadai kuwa endapo wataendelea na kasi hii, basi huenda wakawa miongoni mwa mastaa wakubwa wa Afrika Mashariki katika miaka michache ijayo.

Kwa sasa, ‘Inawauma’ inapatikana kwenye majukwaa yote ya kusikiliza muziki mtandaoni, na mashabiki wanahimizwa kuendelea ku-stream na ku-share ngoma hiyo ambayo tayari imeanza kuwasha moto kwenye playlists za Afrika Mashariki.

Unaweza Kutazama Kusikiliza Wimbo Wao Hapa – https://youtu.be/OzxAWTk_6yE?si=wvs4ljhgmuKMczE8