Trump na Zelenskyy wakutana kwenye mazishi ya Papa Francis

Kabla ya kuanza kwa ibada ya mazishi ya Papa Francis, viongozi nchi mbalimbali walikutana katika Basilica la St. Peter, huku mazungumzo ya ghafla yakifanyika kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump, na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy.

Picha za kipekee zilionyesha viongozi hao wawili wakiongea kwa karibu wakiwa wamekaa katika viti, Inaelezwa kuwa viongozi hao wawili watakutana tena baadaye leo.

Picha nyingine ziliowaonesha viongozi hao wakiongea pamoja na Kiongozi wa Chama cha Labour cha Uingereza, Sir Keir Starmer, na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.