Tundu Lissu Afikishwa Mahakama ya Kisutu

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jioni hii.

Mwanasiasa huyo alikamatwa jana, Aprili 9, 2025, katika wilaya ya Mbinga, mkoa wa Ruvuma, muda mfupi tu baada ya kumaliza kuzungumza kwenye mkutano wa hadhara, na kisha kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma mapema leo imeeleza kuwa Lissu, anatuhumiwa kwa kosa la kufanya uchochezi wa kutofanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Endelea kufuatilia kurasa zetu kwa Taarifa zaidi