Tundu Lissu ahamishiwa Gereza la Ukonga

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa leo, tarehe 19 Aprili 2025, viongozi wakuu wa chama hicho wamekutana na uongozi wa Jeshi la Magereza na kufahamishwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu amehamishiwa katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam

Taarifa iliyotolewa na chama hicho imeeleza kuwa sasa familia, wanachama wa CHADEMA na Watanzania wote waliokuwa na wasiwasi kuhusu mahali alipo Mheshimiwa Lissu, wanaweza kumtembelea kwa kufuata taratibu za kawaida za kumuona mahabusu katika Gereza la Ukonga

Aidha, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mheshimiwa John Heche, anatarajiwa kufika gerezani leo kwaajili ya kumwona Lissu na kuzungumza naye kuhusu hali yake.