Tundu Lissu asomewa Shtaka la Uhaini

Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Antiphas Lissu leo Aprili 10, 2025 amerudishwa mahabusu baada ya kusomewa shitaka la uhaini katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushindwa kujitetea kutokana na kosa hilo kumnyima dhamana na nafasi ya kujitetea.

Lissu amesomewa shitaka hilo leo mapema kabla ya kusomewa mashtaka mengine matatu katika kesi ya pill ya Jinai, likiwemo la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani, Twitter) na kauli za kisiasa. mashtaka ambayo Lissu aliyakana.

Aidha, kutokana mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhaini, kesi hiyo ya kwanza ya uhaini itasikilizwa mahakama Kuu, huku kesi ya jinai ikiahirishwa hadi Aprili 24 mwaka huu.

Lissu alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara, ambapo alisafirishwa hadi Dar es Salaam na kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo.

Upande wa utetezi katika Kesi hizo, unaongozwa na Wakili
Dk Rugemeleza Nshalla, Michael Lugina, Jebra Kambole, Hekima Mwasipu, Dickson Matata na Gastoni Garubindi.