Wazazi waua mtoto kwa kipigo wakimtuhumu kuiba TV

Katika hali isiyo ya kawaida wazazi wa mtoto Bright Joel Malila, Bwana Joel Malila kwa kushirikiana na mkewe wameua mtoto wao kwa kipigo waki mtuhumu kuiba TV ya nyumbani kisha kutokomea kusikojulikana.

Majirani wa Bwana Joel Malila wamesema siku ya tukio walisikia kelele wazazi wakimuadhibu mtoto huyo zilizo sikika kwa muda mfupi sana na wao wakijua ni hali ya kawaida kwa mzazi kufanya hivyo lakini baadae waliitwa na kushtushwa na kile walichokiona.

Wamesema walipo ingia ndani walikuta mtoto akiwa chini na hali mbaya na kumuita balozi na mwenyekiti wakamchukua mtoto na kumpeleka hospitali ambapo muda mfupi baadaye walipewa taarifa za kwamba mtoto huyo amefariki.

Alex Mwalukasa ni polisi kata, kata ya Iganzo amewaomba wananchi wa kata hiyo kutoa taarifa mapema pindi wanapoona daliliza ukatili ili kuzuia matukio ya namna hiyo, huku mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa igodima akiwaomba wananchi hao kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi.