OMO awasilisha hati za kiapo Mahakamani

Mgombea wa Nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya ACT-Wazalendo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Septemba 08, 2025, amewasilisha Hati ya Kiapo, mbele ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Hati hizo ambazo ni sehemu ya fomu za uteuzi wa kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar, zimepokelewa na kuapishiwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar, iliyopo huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja, na Jaji wa Mahakama hiyo, Mhe. Said Hassan Said, ikishuhudiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah.