Mwenge wawasili Geita, Miradi ya Bilioni 164 Kukaguliwa


Mwenge wa Uhuru umewasili mkoani Geita ukitokea mkoani Mwanza, ambapo umepokelewa katika Kijiji cha Rwezera, Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa mbio za mwenge huo ndani ya mkoa huo.

Akizungumza mara baada ya kupokea Mwenge huo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigella, alisema kuwa Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika halmashauri zote sita za mkoa huo, na utakagua jumla ya miradi 61 yenye thamani ya Shilingi bilioni 164.

Mhe. Shigella ametoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Geita kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru na kushiriki katika shughuli za uzinduzi, ukaguzi, na uwekaji wa mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo