Vyama 17 vya siasa vimepeleka wagombea urais wa Zanzibar kwajili ya kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mheshimiwa Jaji Goerge Joseph Kazi amethibitisha kupokea barua za wagombea hao kutoka vyama 17 vya siasa huku akisema kwasasa wagombea hao watatakiwa kutafuta wadhamini na kurudisha fomu kama ilivyolekezwa
Vyama vilivyopeleka wagombea wa Urais wa Zanzibar na kupewa fomu hizo ni pamoja na Chama cha Mapinduzi CCM, ACT-Wazalendo, CCK, NRA, NCCR-MAGEUZI, NLD, DP, ADC, Chama Makini, SAU
Vingine ni UPDP, ADA-Tadea, AAFP, UDP, UMD, TLP na Chama cha wananchi CUF
Vyama 17 vyachukua fomu Urais wa Zanzibar, CHADEMA & CHAUMMA hawajajitokeza

Leave a Reply