Uchaguzi Mkuu 2025 Kugharamiwa kwa Fedha za ndani

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewafahamisha Watanzania kuwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 utagharamiwa kikamilifu kwa fedha za ndani.

Kauli hiyo ameitoa Juni 12, 2025, Bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

“maeneo mengine mahsusi ya vipaumbele ni pamoja na ugharamiaji wa: Deni la
Serikali; mishahara na stahiki za watumishi wa umma; pamoja na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027. Aidha, nipende kuwafahamisha watanzania kuwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025
tutaugharamia kwa fedha zetu za ndani.” – Dkt. Mwigulu