Uingizaji wa Kuku na Samaki kuongezewa Ushuru Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwaka wa fedha 2025/2026 imependekeza kuongeza kiwango cha ushuru wa bidhaa ya kuku na samaki wanaoingizwa nchini kutoka nje nchi kwa gharama ya shilingi 1,000 kwa kilo moja kutoka shilingi 300 iliyokuwa awali

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mheshimiwa Dkt Saada Mkuya Salum ameeleza hayo wakati akisoma Bajeti kuu ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 2025/2026 katika Baraza la Wawakilishi lililopo Chukwani Zanzibar

Dkt. Mkuya amesema uamuzi huo unalenga kuimarisha uzalishaji wa ndani na kuwa na ushindani wa haki katika soko pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi wa Zanzibar

Pamoja na hatua hiyo mapendekezo mengine yanalenga kuongeza kiwango cha shilingi 50 kwa lita moja ya maji safi na salama yanayoingia Zanzibar na kutoza kodi ya miundombinu kwa uingizaji wa tray moja ya mayai kwa kiwango cha shilingi 1,000