Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso umeivunja Tume huru ya Uchaguzi (CENI), ukidai kuwa chombo hicho kilikuwa kikihusika na ufujaji wa fedha. Wizara ya mambo ya ndani ndiyo sasa itasimamia masuala yote yanayohusu uchaguzi katika siku zijazo, kama ilivyoripotiwa na runinga ya taifa, RTB
Tangu utawala huu wa kijeshi ulipoingia madarakani mnamo Septemba 2022, umefanya mabadiliko makubwa. Mojawapo ya maamuzi muhimu ni kuahirisha uchaguzi ambao ungetarajiwa kurudisha nchi kwenye utawala wa kiraia.
Uchaguzi mkuu ulitarajiwa kufanyika mwaka jana, lakini serikali ya kijeshi imepanua muda wa mpito kuelekea demokrasia hadi Julai 2029. Uamuzi huu unampa nafasi Kapteni Ibrahim Traoré, kiongozi wa sasa, kusalia madarakani na pia anaruhusiwa kugombea katika uchaguzi ujao wa urais.
Shirika la habari la AFP limemnukuu Waziri wa Utawala wa Wilaya, Emile Zerbo, akibainisha kuwa tume ya uchaguzi iliigharimu serikali takriban dola 870,000 kwa mwaka.
Leave a Reply