Uwanja wa Benjamin Mkapa wafungiwa kwa Muda

DCIM100MEDIADJI_0038.JPG

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza kuufunga uwanja wa Benjamin
Mkapa kwa muda kuanzia leo tarehe 9 Aprili 2025 ili kupisha marekebisho ya eneo la kuchezea
(Pitch) lililopata athari kubwa kufuatia mvua zilizonyesha na kufuatiwa na mchezo wa Robo
Fainali wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba SC na Al Masry ya Misri.

Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imeeleza kuwa Timu ya Wataalamu itaanza mara moja kufanya tathmini ya kina ya madhara yaliyojitokeza na tarehe ya kufunguliwa kwa uwanja huo itatangazwa hapo baadaye.

Timu zote ambazo zilipanga kuutumia uwanja wa Benjamin Mkapa zikiwemo zinazoshiriki mashindano ya Kimataifa zimeombwa kutafuta uwanja mbadala wakati
Serikali ikifanya marekebisho ya eneo la kuchezea kwa dharura

“Wizara inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na kufungwa kwa uwanja huu
kwa sasa.” – imeeleza taarifa ya Wizara