Vyama vya siasa vya upinzani 14 vimekutana na kuunda jukwaa la pamoja ambalo litajadili ajenda mbalimbali za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, 2025, kwa lengo la kuhakikisha wanakiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.
Katika taarifa yao waliyoitoa leo, Juni 1, 2025, jijini Dodoma kwa waandishi wa habari, uongozi wa vyama hivyo umesema unasubiri ratiba za mikutano mikuu ya vyama vyote ikamilike ili wapate muafaka juu ya iwapo watatumia mfumo wa kumsimamisha mgombea mmoja wa nafasi ya urais au vinginevyo.
Jukwaa hilo la vyama 14 vya siasa limesema kuwa vyama vyao bado vinaendelea na mikutano mikuu, na ajenda yao katika mikutano hiyo ni kujadiliana kuhusu kuungana.
Abdul Mluya kutoka Chama cha DP amesema kuwa katika muungano huo wataangalia ni wa aina gani—kama wa dhahiri au wa siri—na zote ni mbinu za kimkakati kuhakikisha kwamba katika uchaguzi huu CCM inaondolewa madarakani.
Hata hivyo, katika jukwaa hilo la vyama 14 vya siasa, chama cha CHAUMMA, ambacho hivi karibuni kimeonekana kikivutia
Leave a Reply