Team ya Waandishi wa Habari akiwemo Mwandishi wa Habari kutoka Wasafi Media @hamisimguta na waandishi wanne wa wa 7seven Media waliokuwa wakisafiri kutoka mkoani Kigoma kuelekea jijini Dar es Salaam imepata ajali katika eneo la Bwawani mkoani Morogoro, wakiwa na gari aina ya Alphard.
Kwa mujibu wa taarifa za awali ajali hiyo imetokea kufuatia gari hiyo kuchomekewa na gari aina ya Lori, ambapo waandishi hao baadhi wamepata majeraha madogo madogo na wote wanaendelea vizuri, wakiendelea na taratibu za matibabu na kisha kuendelea na safari kwa msaada wa jeshi la Polisi.

Leave a Reply