Jamii ya Wahadzabe, waokota matunda na wala nyama wanaoishi katika mikoa ya Arusha, Manyara, Singida na Simiyu, wamepaza sauti kulalamikia vitendo vya baadhi ya watengeneza maudhui ya mtandaoni vinavyokiuka mila na tamaduni zao.
Wanasema wamekuwa wakilazimishwa kurekodiwa katika mazingira yanayowadhalilisha na kupotosha taswira ya maisha yao ya kiasili.
Malalamiko hayo yametolewa katika jumuiko la jamii hiyo lililofanyika wilayani Karatu, ambako wameeleza kuwa baadhi ya maudhui yamekuwa yakisambazwa kwenye mitandao ya kijamii yakiwaonyesha wakila nyama mbichi na kushiriki vitendo vinavyotafsiriwa kama kudhalilisha utu wa binadamu.
Leave a Reply