WAKILI AOMBA KESI YA BIL 26 YA TREY SONGZ IFUTWE

Wakili wa Staa wa Muziki #Treysongz amewasilisha ombi mahakamani akitaka jaji kufuta hukumu ya dola milioni 11 -Tsh.Bilioni 26+ ambazo mwimbaji huyo aliamriwa kumlipa afisa wa zamani wa polisi aliyedaiwa kushambuliwa naye.

Kulingana na nyaraka zilizopatikana #Trey anadai hakujua kuhusu kesi hiyo hadi taarifa za hukumu hiyo zilipotangazwa kwenye mitandao ya kijamii mwishoni mwa Novemba.

Wakili wake anasema #Trey anastahili kupata haki yake mahakamani kwani kulazimika kulipa kiasi hicho kutaharibu maisha yake.

#TreySongz aliamriwa kulipa dola milioni 11 baada ya Afisa wa zamani wa Maryland Capital, #TyrellDunn, kudai kwamba Trey alimpiga. #Dunn anadai kwamba mke wake alikuwa amealikwa katika chumba cha hoteli cha Trey mwaka 2021.

Pia alidai kuwa alipojaribu kumchukua Mke wake alipigwa na #Trey Mpaka kupelekea kuumia maeneo ya jicho.