Wamandoa wawili ambao ni Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wameawa na wananchi wa kijiji cha chafuma kata ya kapele tarafa ya ndalambo Wilayani Momba Mkoani Songwe Agosti 22,2025.
Raia hao wanadaiwa walioingia nchini kinyemela bila kufuata utaratibu wa kisheria ambapo tukio hilo lililotokea tarehe 22 Agosti 2025, saa 8:00 mchana, katika Kijiji cha Chafuma, Kata ya Kapele, Tarafa ya Ndalambo, Wilaya ya Momba.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa
Wa Songwe Kamshina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema Marehemu hao ni Babuloha aliyefahamika kwa jina moja mwenye umri kati ya miaka 26 hadi 28, na Jenifa Babuloha, mwenye umri kati ya miaka 23 hadi 25, wanandoa ambao waliuawa kikatili kwa kupigwa na kuchomwa moto na wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi wakiwatuhumu kuhusika na mauaji ya Imbanji Simwaka, mwanamke kikongwe mwenye umri wa miaka 80 ambaye alikuwa mwenye nyumba wao.
Tukio hilo lilitokea usiku wa tarehe 19 Agosti 2025, ambapo Imbanji Simwaka aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani, na mwili wake kufukiwa bafuni nyumbani kwake, na tangu tarehe 20 Agosti 2025 marehemu hakuonekana, hali iliyozua wasiwasi miongoni mwa ndugu na wanakijiji.
Kutokana na kutoonekana kwake ndipo wanakijiji walianza kumtafuta na ilipofika tarehe 22 Agosti 2025 waligundua kaburi la siri bafuni na wakaanza kusambaza taarifa kuwa wanandoa waliopanga chumba kwa marehemu walikuwa wakiuza baadhi ya mazao ya marehemu, jambo lililoibua mashaka na hasira kwa jamii, ndipo wananchi waliwakamata wanandoa hao na kuwakabidhi kwa uongozi wa kijiji kwa ajili ya taratibu za kisheria.
Aidha Kamanda amesema Uchunguzi wa kina unaendelea ili kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wote waliopanga, kushiriki au kuchochea tukio hili la mauaji.
Mwisho
Wanandoa raia Wa Congo Wauawa Kwa Kupigwa Na Kuchomwa Moto Songwe

Leave a Reply