Watu 25 Wadakwa Kwa Tuhuma Za Makosa Ya Kimtandao | Wakitumia Tiktok Na Akili Mnemba ‘AI’

Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watu 25 kwa tuhuma za Makosa ya kimtandao katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo na mikoa mingine ya Jirani.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP. Jumanne Muliro akizungumza leo Machi 07, 2025 ameeleza kukamatwa kwa mtu aliyetajwa kwa majina ya Kelvin Sauro kwa akituhumiwa kuongoza kikundi cha kihalifu mtandaoni, kutumia laini za simu zisizo na usajili wao, kuingilia na kubadili namba za utambuzi halisi wa simu, (IMEI), kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu pamoja na kujifanya maoafisa wa mfuko wa penheni na kisha na kuwaibia wastaafu.

“Pia wamekuwa wakitenda makosa ya utakatishaji wa fedha, Watuhumiwa hawa wamekuwa wakituma jumbe kama, tuma ile hela kwa namba hii au tuma kwenye namba hii ile pesa ya kodi, au Leta namba za NIDA, Vitambulisho tukushughulikie mapunjo yako ya kustaafu” amesema SACP Muliro.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi linamshikilia pia Enrique Adolph Ngagani na wenzake wanne wakazi wa Sinza Jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za kumiliki akaunti za mtandao wa Tiktok zinazotumika kusambaza taarifa zenye maudhui ya udhalilishaji wa watu mbalimbali kupitia Program za akili Unde (AI).