Watu Saba wafariki, Wengine 42 wajeruhiwa Katika Ajali ya Basi Mwanga

Watu Saba wamefariki dunia na wengine 42 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Mvungi Trans kuacha njia na kupindukia mtoni katika kijiji Msangeni kata ya kifula wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro.


Akithibitisha juu ya ajali kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro Simon Maigwa amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva kukosa umakini kwenye kona hali ambayo ilimpelekea kushindwa kuhimili kasi ya gari na kuacha njia.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya wilaya huku wengine wakipelekwa katika hospitali ya Mawenzi na KCMC.

Video kuhusu Ajali iliyoua Watu 7 Wilayani Mwanga


Ajali hii imetokea ikiwa ni siku chache zimepita gari lingine aina ya coaster ku1acha njia na kupinduka na kuua wanakwaya sita katika wilaya ya Same.