Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka halmashauri zote hapa nchi kufanya jitihada za makusudi kupunguza uzalishaji wa taka kwenye maeneo yao, ikiwemo kuja na mipango ya kuiwezesha jamii kushiriki katika biashara ya kaboni.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo leo mei 03, 2025 wakati akizungumza katika Kongamano la Vijana lililokuwa na lengo la kuwapatia fursa ya kutoa ushauri juu ya namna ya kukabiliana na mabadidiriko ya tabianchi.
Amesema Serikali imeendelea kutekeleza mipango ya kuweza kukabiliana athari mbaya ya Mabadiliko ya tabianchi kwa kuongeza Msukumo katika kupanda miti kwenye halmashauri zote.
Aidha, Majaliwa amewataka vijana hao kutumia kongamano hilo ili kuweza kufikia malengo ya serikali juu ya mapambano ya mabadiliko ya tabia nchi hapa nchini.
Leave a Reply