Wimbo Wa Jux Na Phyno ‘God Design’ Ndani Ya Top 10 Itunes Nigeria

Msanii kutoka Tanzania Juma Jux, Anafanya Vizuri Kwenye soko la muziki la kimataifa baada ya ngoma yake mpya “God Design” aliyomshirikisha staa wa Nigeria, @phynofino 🇳🇬, kushika nafasi ya 9 kwenye chati za iTunes Nigeria.

Wimbo huu umeibuka kuwa moja ya nyimbo zinazopigwa sana nchini humo, na umekuwa gumzo kwenye redio, mitandao ya kijamii, na majukwaa mbalimbali ya burudani, ikiashiria kuwa Jux anazidi kutanua wigo wake Upande Afrika Magharibi.

Hii ni dalili tosha kuwa Jux kwa sasa Anazidi Kufanikiwa kwenye soko la Nigeria, huku “God Design” ikionekana Kuwa Moja Ya Njia Ya mafanikio yake kwenye ukanda huo wa muziki, Baada Ya Ololufe Mi, Enjoy Ambazo Pia Zimekuwa Zikisumbua Upande Huo Wa Africa Magharibu (Nigeria, Ghana N.K).