Yammi Aacha Na Label Ya Nandy ‘The African Princess’.

Msanii Wa Bongo Fleva Nchini @officialnandy Ameweka Wazi Kuwa Msanii Wake @yammitz Rasmi Amemaliza Mkataba Wake Na Label Yake Ya ‘The African Princess’ Na Kupata Wawekezaji Wapya Watakaoendeleza Kipaji Chake.

“African Princess Records inapenda kuwataarifu rasmi wadau wa muziki, vyombo vya habari, na mashabiki wote kuwa msanii wetu mpendwa Yasirun Yasin Shaban, anayefahamika zaidi kwa jina la kisanii Yammi, ameihitimisha rasmi mkataba wa usimamizi wa kazi zake na lebo yetu ya The African Princess Label kwa makubaliano ya kirafiki na kwa manufaa ya pande zote mbili.

Tunaamini kuwa lebo imetoa mazingira bora yaliyo mwezesha Yammi kukua na kupevuka kisanaa, na tunafurahia kuona kuwa sasa amepata wawekezaji wapya waliovutiwa kuendeleza na kusimamia zaidi kipaji chake na kumsaidia kufikia hatua kubwa zaidi kimataifa” – Label Ya The African Princess

Barua Ya Label Ya The African Princess Ikiweka Wazi Kuachana Na Yammi.