Yanga yamwaga mamilioni kunasa saini ya Moussa Conte

Klabu ya Yanga imethibitisha kumsajili Kiungo wa CS Sfaxien ya Tunisia, Moussa Balla Conte (21).

Nyota huyo raia wa Guinea ambaye pia alikuwa akiwaniwa na Wekundu wa Msimbazi, Simba SC ametua Mitaa ya Twiga na Jangwani kwa dau la USD 250,000 zaidi ya milioni 651 za kitanzania.