Yanga yasisitiza haitacheza Derby

Uongozi wa Klabu ya Yanga leo Juni 9, 2025 imekutana na Uongozi wa Bodi ya Ligi na kuzungumzia juu ya sakata la msimamo wa kutotaka kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Simba mchezo ulioahirishwa hapo awali.

Kupitia Barua ya wazi ya Yanga wameeleza kuwa baada ya majadiliano ya saa kadhaa, Viongozi wa Klabu waliwasilisha msimamo wa klabu kuwa Yanga haitashiriki mchezo namba 184 uliopangwa kufanyika Juni 15, 2025 hadi pale matakwa yao waliyoyawasilisha kwa maandishi kwa badi ya Ligi yatakapotimizwa