Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 73 wa Viwanja vya ndege Afrika

Tanzania inatarajiwa kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 73 wa Baraza La viwanja vya Ndege la Kimataifa Kanda ya Afrika (ACI) utakaofanyika kuanzia Aprili 21-30 jijini Arusha ukihudhuriwa na Wajumbe zaidi ya 400 ndani na Nje ya Afrika.

Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema Hayo mbele ya Waandishi wa Habari jijini Arusha wakati akieleza namna Tanzania ilivyojiandaa na mkutano huo.

Amesema Miongoni mwa Manufaa ambayo Tanzania itanufaika nayo ni kuongezea Ujuzi kwa Wazawa kuhusu masuala ya Anga na Utalii.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amesema ujio wa Mkutano huo ni fursa kwa Wananchi kwa kuwa uchumi wao unakwenda kuchangamka Zaidi.

Baraza La Ndege la Kimataifa Kanda ya Afrika, lenye Makao makuu yake nchini Morocco, lina Wanachama 75 wenye viwanja 265 katika mataifa 54 pamoja na Mashirika 59 ya Ndege barani Afrika.