Lyanga mbadala wa Mgunda ndani ya Mashujaa FC

Kuna taarifa kwamba klabu ya Mashujaa FC kutoka Kigoma, inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, inahusishwa na usajili wa mshambuliaji kutoka JKT Tanzania, Daniel Lyanga. 

Inasemekana Mashujaa wanahitaji huduma ya Lyanga kama mbadala wa Ismail Mgunda ambaye anatajwa kujiunga na AS Vita ya DR Congo.

Lyanga mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Simba, Geita Gold na JKT, amekuwa akihusishwa na vilabu mbalimbali katika kipindi hiki cha usajili.

Kwa sasa bado hakuna uthibitisho rasmi wa kujiunga kwake na Mashujaa FC.