Mshambuliaji wa Mashujaa FC, Ismail Mgunda, yuko mbioni kujiunga na klabu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kwa mujibu wa taarifa, Mgunda amesaini mkataba wa miaka miwili na AS Vita, baada ya mazungumzo kati ya klabu hizo mbili.
Mgunda, mwenye umri wa miaka 29, amekuwa na mchango muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Mashujaa FC, akifunga mabao mawili msimu huu.
Kocha wa AS Vita, Youssouph Dabo, ambaye aliwahi kuifundisha Azam FC, amemwona Mgunda kama mchezaji anayefaa kuimarisha kikosi chake.
Kwa sasa, inasubiriwa Mgunda kusafiri kwenda DR Congo kwa ajili ya vipimo vya afya na kukamilisha taratibu za usajili. Iwapo kila kitu kitakwenda vizuri, atajiunga rasmi na AS Vita katika siku chache zijazo.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.