Michuano ya CHAN 2024 yasogezwa mbele hadi Agosti 2025

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limethibitisha kusogeza mbele michuano ya CHAN 2024 hadi Agosti 2025 ambapo awali ilipaswa kuanza kutimua vumbi kuanzia Februari 1-28, 2025 katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Chanzo cha kusogezwa mbele kwa michuano hiyo ni ukosefu wa miundombinu, ukosefu wa vifaa, ukosefu wa viwanja, kushindwa kupata timu kamili ambapo kwa sasa zipo timu 17 kati ya 19 zinazotakiwa.

CAF imeamua kucha ligi zote za Afrika kumaliza msimu wa 2024/25 pia kutoa muda na wa kutosha wa maandalizi kwa timu  za taifa kama Algeria, Misri na Afrika Kusini kujiandaa kwa mechi za mtoano na kuamua ni nani atafuzu.