Alexander-Arnold kujiunga na Real Madrid majira ya joto

Miamba ya Uhispania Real Madrid wameripotiwa kukata tamaa ya kumpata Trent Alexander-Arnold (26) kwenye klabu yao msimu huu wa baridi baada ya dalili kutoka kwa mchezaji huyo ambaye amechagua kumaliza msimu huu (2024/25) akiwa na Liverpool.

Beki huyo wa kulia wa Liverpool alipewa ofa ya mkataba mpya na Wekundu hao mwanzoni mwa dirisha la usajili lakini bado hajamwaga wino kuongeza muda wa kuitumikia Liverpool.

Hata hivyo, Liverpool hawana nia ya kumuuza katikati ya msimu huku wakati Alexander-Arnold pia anataka kusubiri hadi majira ya joto hivyo anaweza kujiunga na Real kama mchezaji huru, isipokuwa kama atatia saini mkataba mpya wa Liverpool.

Aidha zipo taarifa kwenye baadhi ya vyanzo vya habari kuwa Alexander-Arnold na Real Madrid tayari wameshafanya mazungumzo na wamefukia makibaliano ya mdomo kuwa mchezaji huyo atajiunga na Real Madrid dirisha kubwa.

#WasafiSports