Achraf Hakimi amesaini mkataba mpya na Paris Saint-Germain (PSG) ambao utamuweka klabuni hapo hadi Juni 2029.
Tangu alipojiunga na PSG mwaka 2021, Hakimi amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi hicho, akionyesha uwezo mkubwa chini ya kocha Luis Enrique.
Katika msimu huu, amecheza mechi 13, akifunga mabao mawili na kutoa pasi tatu za mabao.
Mkataba huu mpya unaonyesha dhamira ya PSG ya kuimarisha kikosi chake kwa kuzingatia wachezaji wenye mchango mkubwa kama Hakimi.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.