Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limeitangaza Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kuwa Ligi ya nne (4) kwa ubora barani Afrika na ya 57 duniani kwa mwaka 2024.
Ligi hiyo imepanda kwa nafasi mbili (2) kutoka nafasi ya sita (6) mwaka 2023 ikizipiku Ligi za Afrika Kusini na Tunisia.
Misri wanaongoza kwa ubora Afrika, wakifuatiwa na Morocco, nafasi ya tatu ni Algeria, Tanzania nafasi ya nne na Tunisia nafasi ya tano.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.