Universal Music Group imechukua hatua kali dhidi ya kesi ya Drake, ikitafuta kutupiliwa mbali kwa kesi hiyo iliyofunguliwa Texas.
Label hiyo ya muziki imewasilisha ombi lenye kurasa 144 likitaka kesi hiyo ifutwe, ikikanusha madai yote ya ukiukwaji wa sheria na kuielezea kama hatua ya kisasi kutoka kwa Drake. Pia, UMG imeomba kusitishwa kwa uchunguzi wa kisheria na malipo ya ada za kesi, ikisisitiza kutotaka kugharamia madai ya msanii huyo kutoka Toronto.
Kwenye ombi hilo, UMG imemshutumu Drake kwa hatua ya kimkakati ya kisasi cha kisheria dhidi ya UMG na wengine, huku wakidai kuwa kuna juhudi za kuzuia usambazaji wa wimbo “Not Like Us.”
Hatua hii imechukuliwa siku chache kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo Januari 28, huko Bexar County, Texas. Kesi ya Drake dhidi ya UMG inazidi kuwa na mvutano, huku label hiyo ikiwa imepewa nyongeza ya siku 34 kujibu mashtaka kutokana na moto wa porini huko Los Angeles uliodaiwa kuathiri timu za kisheria na utendaji za UMG.
Mwanasheria wa UMG, Nicholas Crowley, alisema, “Tunaomba nyongeza hii kwa sababu moto wa porini huko Los Angeles umeathiri sana timu za utendaji na kisheria za mshtakiwa.”
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.