Emery aifukuzia saini ya Foyth wa Villareal

Mkufunzi wa Aston Villa, Unai Emery yuko tayari kumnunua mlinzi wa Villarreal, Juan Foyth (27) huku akitafuta beki mpya wa kati ili kuimarisha safu yake ya ulinzi kabla ya mwisho wa dirisha la uhamisho la Januari baada ya Diego Carlos kuhamia Fenerbahce na Pau Torres kuumia.

Villa wamehusishwa na mlinzi huyo wa zamani wa Tottenham, ambaye alicheza chini ya Emery huko Villarreal, na Mhispania huyo inaelewa hangeweza kukataa kujiunga na Villa.

“Ni kweli namfahamu Juan Foyth kwa sababu nilifanya naye kazi. Ni mchezaji mmoja mzuri sana kwa ubora wake anaweza kuungana na kucheza akiwa na sifa na kiwango tunachotaka kuongeza kikosini,” alisema Emery.