Joyner Lucas ameweka wazi nia yake ya kurudi kwenye mashindano ya rap kwa kumchokoza rapa Meek Mill. Hii imejiri baada ya Lucas kuandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) akisema:
“Wakati mwingine najikuta natamani kurudi kwenye ulingo wa URL battle rap.”
Ultimate Rap League (URL), moja ya majukwaa makubwa ya battle rap, walijibu kwa kuonyesha utayari wao, wakisema:
“Tufanye kazi hiyo.”
Pamoja na kwamba #JoynerLucas mwanzo alikubali kupambana na yeyote atakayependekezwa na URL, aliamua kuweka pendekezo lake. Aliandika:
“Ningependa nijaribu raundi moja kwanza ili kuzoea. Ningependa pia kupambana na msanii mwenzangu ambaye hana uzoefu mkubwa wa battle rap lakini ana uwezo wa kisanaa. Lakini, kwa upande mwingine, kupambana na mtaalamu wa muda mrefu kunaweza kuwa sehemu ya burudani.”
Hatimaye, Joyner Lucas alimtaja Meek Mill kama chaguo lake kwa kusema:
“Vipi @meekmill.”
Mashabiki wanasubiri kuona kama #MeekMill atajibu hii na kama battle rap itafanyika.
Unafikiri ni nani mkali kati ya Joyner Lucas na Meek Mill?
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.