Ded Siha azindua kitabu cha malezi ya watoto zama za kidijitali

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Siha Haji Mnasi hatimaye amezindua kitabu cha elimu na malezi kwa Watoto katika zama za Kidijitali yenye lengo la kutoa elimu kwa wazazi na watoto jinsi juu ya malezi katika zama za digitali.

Akizungumza wakati uzinduzi wa Kitabu hicho ambacho kimezinduliwa katika kijiji cha Kitangari B kilichopo wilayani Newala mkoani Mtwara, Uzinduzi, Dkt Mnasi amemshukuru raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kumuamini

Huku akisema licha ya Kuwa na majukumu mengi ya kiserikali ila aliwiwa kuandika kitabu hicho cha Elimu na malezi kwa watoto katika zama za kidijitali kutokana na Kasi kubwa ya ukuaji wa utandawazi ambao Kwa kiwango kikubwa unaathiri Mila na tamaduni Kwa Jamii.

Amesema kitabu hicho kinaenda Kuwa suluhisho katikati zama hizi za utandawazi huku akiwataka wazazi, walezi pamoja na jamii kusoma kitabu hicho ili kuwasaidia watoto katika namna Bora ya kujifunza na kupata elimu pamoja na malezi yaliyo bora

r