Grammy Wamuomba Msamaha Mwanamuziki The Weeknd .

Miaka Minne (4) Iliyopita Mwanamuziki “The Weeknd” Aliripotiwa Kama Muhanga Wa Tuzo Za Grammy Baada Ya kuwatupia lawama kwamba ni wala rushwa mara baada ya jina lake kukosekana kwenye vipengele vyote vya tuzo hizo 2021. Sio Hivyo Tu #TheWeeknd Aliweka Mgomo Wa Kutowasilisha Kazi Zake Lakini Pia Kutoshiriki Tena Katika Tuzo Hizo.

Tweet Ya The Weeknd Ya Mwaka 2020 Akidai Grammy Zimejaa Rushwa.

Sasa Usiku Wa Feb 2(Jana Jumapili) Mkurugenzi Wa Tuzo Za Grammy Harvey Mason Ambaye Pia ni miongoni mwa wana jopo la Recording Academy ambalo uhusika kwenye kuchuja na uteuzi wa majina ya wasanii kuingia kwenye vipengele, amezungumza Juu Ya Sakata Hilo La The Weeknd Kuzigomea Tuzo Hizo, Ambapo Aliweka Wazi Kuelewa Madai Ya The Weeknd Na Hivyo Kumaliza Tofauti Zao Kwa Kuyafanyia Kazi Lakini Pia Hakuamini Kama Muimbaji Huyo Angeweza Kutumbuiza Tena Katika Hafla Ya ugawaji Wa Tuzo Hizo.

“Sikuwa Na Uhakika Kama Huyu Jamaa Atapanda Tena Katika Jukwaa La Grammy, Marafiki Pamoja Na Wanamuziki Naomba Tumkaribishe Tena The Weeknd” – Harvey Mason (CEO Wa Grammy)

Mkurugenzi Wa Tuzo Za Grammy Harvey Mason Jr.

Show Ya The Weeknd Ambayo Ilikuwa Kama Suprise Katika Tuzo Za Grammy 2025 Ndio Inakuwa Show Yake Ya Kwanza Tangu 2021 Alivyozisusa Tuzo Hizo.