Mshukiwa Wa Mauaji Ya Pop Smoke Akiri Makosa .

Mmoja Kati Ya Washukiwa wanne wa mauaji ya #PopSmoke yaliyotokea Feb 2020 huko Hollywood Hills, amekiri kosa la mauaji bila kukusudia. Kwa mujibu wa @kcalnews, #CoreyWalker( 24) amekiri makosa mawili ya wizi/ Uvamizi wa kuvunja nyumba (Robbery).

Awali Walker alishtakiwa kwa mauaji na alikabiliwa na kifungo cha maisha jela Bila uwezekano wa kupatiwa msamaha .

Walker alikuwa na umri wa miaka 19 wakati mauaji ya pop smoke yalipotokea. Hivyo kwaSasa anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 29 Jela. Hukumu Ya Walker Itatoka Feb 21, 2025 .