Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua kituo chenye mtambo mpya na wa kisasa wa ukaguzi wa vyombo vya moto visiwani Zanzibar.
Kituo hicho kilichogharimu takribani shilingi bilioni 2.8 kina uwezo wa kukagua magari 400 kwa siku na kinajumuisha eneo la mgahawa, sehemu ya ibada, sehemu ya mafunzo kwa madereva na maeneo mengineyo ambapo gari moja linaweza kufanyiwa ukaguzi ndani ya dakika 15 tu.
Aidha katika kuhakikisha usalama za madereva na watumiaji wa kawaida wa barabara, kituo hicho kimefungwa CCTV camera mpya 70 kwa ajili ya kuangalia usalama.
Uzinduzi wa mtambo huo wa kituo cha KWASILVA chini ya kampuni ya Zenj General Merchandise na uwekezaji wa Mzalendo Turky kwa kushirikiana na makampuni makubwa ya dunia MAHA, DKT na Applaus+ umefanyika leo Februari 11, 2025 katika eneo la Dole, Mkoa wa Mjini Magharibi, Kisiwani Unguja.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.