Kupitia falsafa ya 4R Rais Samia hana ubaguzi katika maendeleo – Nguli

Mkazi wa Kisaki, Mkoani Singida, Samson Nguli amesema kuwa Rais, Samia Suluhu Hassan, hana unaguzi kwenye kuleta maendeleo kwa wananchi wake na ameendelea kutekeleza falsafa ya 4R, Maridhiano (Reconciliation), Mabadiliko (Reform), Ustahimilivu (Resilience) na Kujenga upya (Rebuilding).

“Rais hana ubaguzi katika maendeleo, kwani amejikita katika falsafa ya 4R Kupitia falsafa hii, anahakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa usawa kote nchini bila kujali itikadi za kisiasa. 

“Serikali yake imeimarisha miundombinu, elimu, afya, na nishati, ikilenga kuboresha maisha ya Watanzania wote,” amesema Nguli.