‘Red Card’ ya Bellingham yamuweka refa matatani

Mwamuzi wa mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Osasuna, Munuera Montero amepewa adhabu ya kutochezesha mchezo mwingine mpaka pale ambapo kesi yake itaamuliwa.

shirikisho la mpira la Hispania (RFEF) wameanza uchunguzi ili kubaini kama Kuna maslahi binafsi aliyonayo Munuera Montero baada ya kumtoa Bellingham kwa kadi nyekundu.

RFEF watakagua pia shughuli zake binafsi ili kubaini kama zinahusika na majukumu yake kwenye uamuzi.

Munuera Montero alifanya maamuzi ya kutoa kadi nyekundu kwa Jude Bellingham akidai kwamba alimtukana jambo ambalo limezua taharuki kubwa kwa wachezaji na viongozi wa Real Madrid.