Simba Yatamba Uwanja wa Majaliwa – Yashinda 3-0 Dhidi Ya Namungo

SIMBA YATAMBIA UWANJANI, YAICHAPA NAMUNGO 3-0 – KADI NYEKUNDU YAZUA UTATA

Klabu ya Simba SC imeendelea kuonesha ubabe wake katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuichapa Namungo FC kwa mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa leo. Ushindi huu umewafanya Wekundu wa Msimbazi kuendelea kusalia kwenye mbio za ubingwa huku wakionesha kiwango cha juu, huku mechi ikigubikwa na tukio la kadi nyekundu yenye utata kwa Derrick Mukombozi wa Namungo dakika ya 32.

Mchezo Ulivyokuwa

Dakika ya 32, mchezo ulipata sura tofauti baada ya beki wa Namungo, Derrick Mukombozi, kupewa kadi nyekundu kwa kile kilichoonekana kuwa kuna tukio aliliona amemfanyia mchezaji wa Simba Leonel Ateba na kuamua kusimamisha mpira na kumpa kadi nyekundu. Uamuzi huu ulizua mjadala mkubwa kati ya mashabiki na benchi la Namungo, wakidai kuwa hakukuwa na kosa lililostahili adhabu hiyo kali.

Simba iliendelea mchezo kwa kasi, ikimiliki mpira na kushambulia mara kwa mara lango la Namungo. Haikuchukua muda mrefu kwa mashabiki wa Simba kushangilia baada ya Jean Charles Ahoua kufunga bao la kwanza dakika ya 45+5 kwa penati.

Bao la pili lilifungwa tena kwa penati na mchezaji Jean Charles Ahoua na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 2-0 ndani ya dakika 72 mapumziko.

Kipindi cha pili, Simba iliendelea kutawala mchezo huku wakitafuta mabao zaidi. Juhudi zao zilifanikiwa dakika ya 72 , baada ya Jean Charles Ahoua kufunga bao la pili kwa penati.

Ndani ya dakika ya 90+2 mshambuliaji wa Simba Steven Mukwala alifanikiwa kufunga bao la tatu na kuihakikishia Simba ushindi mnono wa mabao 3 – 0.

Ahoua Ang’ara – Mchezaji Bora wa Mechi

Katika mchezo huu, kiungo wa Simba Jean Charles Ahoua aliibuka kuwa Mchezaji Bora wa Mechi kutokana na mchango wake mkubwa katika safu ya ushambuliaji. Ahoua alihusika katika mashambulizi mengi, akitoa pasi muhimu na kuwasumbua mabeki wa Namungo kwa kasi na umahiri wake wa kumiliki mpira na kufanikiwa kufunga mabao mawili.

Simba Yawapa Mashabiki Furaha

Ushindi huu umeongeza morali kwa mashabiki wa Simba, ambao walijitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao. Kwa upande wa Namungo, walijitahidi kupambana lakini walishindwa kupenya safu ya ulinzi ya Simba, huku kipa wa Wekundu wa Msimbazi akifanya kazi kubwa kuzuia mashambulizi machache ya wapinzani wao.

Msimamo wa Ligi

Kwa matokeo haya, Simba inaendelea kuweka presha kwa vinara wa ligi Yanga huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Unaweza kutazama msimamo wa ligi baada ya matokeo haya hapa chini
Unaweza kutazama msimamo wa ligi baada ya matokeo.