Nyota Wa Muziki Africa SIMBA 🦁 @diamondplatnumz Amefanya Mahojiano Na Kituo Maarufu Cha Redio @hot97 Iliyopo Mjini New York Nchini Marekani. Diamond Amefanya Interview Hiyo Kuelekea Tuzo Za Trace Awards Zikatazofanyika Zanzibar Tarehe 26 Mwezi Huu .
Katika Interview Hii Diamond Amejibu Kuhusu Tuzo Hizi Za Trace Kufanyika Zanzibar Awamu Hii; “Ni Upendeleo Kufanyika Hapa Nchini Tanzania, Na Kama Unavyofahamu (Trace) Ni Jukwaa Kubwa Linalofuatiliwa Na Kutazamwa Na Mamilioni Ya Watu. Mbali Na Kuonesha Vipaji Lakini Tunapata Hata Kuonesha Uzuri Wa Nchi Tuliyonayo Kwa Watu, Hivyo Ina Faida Sana Kwetu Na Hivyo Kuiandaa Tu Ni Upendeleo Wa Kipekee Kwetu”
Diamond Pia Amejibu Kuhusu Muziki Wa East Africa Kutotambulika Duniani Kama Muziki Wa West Africa “Afrobeats” (Ghana, Nigeria), Amapiano (South Africa).
“Ndio Unajua Tunatakiwa Kukubali Kwamba Inachukua Muda, Kwamba Ni Zamu Kwa Zamu Na Hivyo Ndivyo Inavyokuwa. Hatuwezi Kuwa Wote Wakati Mmoja. Unajua Kwamba Tasnia Ya Muziki Kwa Africa Ilianzia Congo Kwanza, Congo Ndio Walikuwa Watu Wa Kwanza Wanaofanya Vizuri Ulimwenguni, Baada Ikafuata Afrika Kusini, Kisha Nigeria … Halafu Ikarudi Afrika Kusini Tena”
“Lakini Pia Amini Ninachokisema tunafuata Sisi… Maana Mwaka Jana Tuliachia Ngoma Nyingi Za Kimataifa Na Kwa Upande Wangu Niliachia Nyimbo Mbili (2) (Shuu & Komasava) Na Uliona Watu Kama Chris Brown Na Jaosn Derulo… Aah Watu Tofuati Kama Travis Scott Alicheza Wimbo Huo Pia… Hiyo Inathibitisha Ni Jinsi Gani Tumeanza Kukuwa, Hivyo Ni Suala Tu La Kuongeza Juhudi Na Kulisoma Soko” – Diamond Platnumz Na @oldmanebro (Hot 97) .
Diamond Platnumz Anatajwa Kuwa Mmoja Kati Wasanii Watakaotumbuiza Kwenye Usiku Wa Tuzo Hizo Pamoja Na Wasanii Wengine Kama Vile Rema, Fally Ipupa, Titom & Yuppe, Zuchu N.k
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.