Dkt. Batilda amkaribisha Rais Samia Tanga kwa ziara ya kikazi

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani amemkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Tanga. 

Ziara hiyo ya kikazi ya Mhe. Rais inaanza leo Februari 23 katika Wilaya ya Handeni ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ataweka jiwe la Ufunguzi katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni iliyopo Mkata na kuzungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkata.