Mbunge wa Jimbo la Buchosa Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Eric Shigongo, amesema Jamii ya Kitanzania inapaswa kutambua kwamba Rais Dkt Samia Suluhu anasalia kuwa Kiongozi Bora kwa wakati huu kwa sababu ya uwajibikaji mzuri ambao anaonesha katika Sekta mbalimbali, huku akifuata nyayo za Watangulizi wake, akiwemo Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Shigongo ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam, leo Februari 22, 2025 katika mkutano wake na Wana habari alipokuwa akielezea masuala kadhaa ya Kitaifa, ikiwemo Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na hali ya Kisiasa hapa nchini.
“Mimi huwa nampima Kiongozi sio kwa Sababu ni kutoka katika Chama changu, bali huwa nampima kutokana na matokeo Chanya katika Ukuaji Uchumi kupitia Takwimu zinazotolewa kupitia maendeleo ya Sekta Mbalimbali, Ukweli uliopo kwa Sasa ni Rais Dkt Samia Suluhu amekuwa kiongozi Bora kutokana na Mchango anaotoa kwenye Sekta mbalimbali na mafanikio yanayoonekana hata kwa Macho tu” amesema Shigongo.
Kuhusu Bunge la Tanzania kuisimamia Serikali, Erick Shigongo amesema limekuwa limekuwa likiisimamia Serikali na ndio maana kumekuwa na Mafaniko Chanya kwenye Miradi mbalimbali ya Maendeleo na Kimkakati.
“Kama hatuisimamii Serikali vizuri, matokeo hayawezi kuwa mazuri, kwa hiyo sifa zote ambazo zinatolewa kwa Serikali ni matokeo ya Mhimili kuisimamia Serikali Vizuri, kwa Sababu Bunge linaongozwa na Spika ambae ni Mchapakazi Dkt Tulia Ackson” ameeleza Shigongo.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.