Karihe afungiwa mechi tatu, faini 500,000

Mchezaji wa Mashujaa FC, Seif Karihe ameadhibiwa kwa kufungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Tsh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Azam FC, Feisal Salum. 

Karihe alimkanyaga Feisal wakati akiwa chini baada ya kumfanyia rafu na adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 41:5 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.